EasyManua.ls Logo

Snapper SPX-100 - Page 110

Snapper SPX-100
120 pages
To Next Page IconTo Next Page
To Next Page IconTo Next Page
To Previous Page IconTo Previous Page
To Previous Page IconTo Previous Page
Loading...
10
Kuwasha Injini
ONYO
Mafuta na mvuke wake yanaweza kuwaka moto
haraka sana na kulipuka.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha majeraha
mabaya ya moto au kifo.
Unapowasha Injini
Hakikisha kwamba plagi ya spaki, kizuia kelele,
kifuniko cha mafuta, na kisafishaji hewa (ikiwa
kunacho) vimefungwa mahali vinapofaa.
Usishtue injini wakati plagi ya spaki imeongolewa.
Ikiwa injini itafurika, weka choki (ikuwa kunayo) katika
upande wa FUNGUA/ENDESHA, sogeza kifaa cha
kudhibiti mmiminiko wa mafuta (ikiwa kunacho)
upande wa HARAKA na ushtue hadi injini iwake.
ONYO
Injini hutoa monoksidi ya kaboni, gesi ya sumu
isiyo na harufu wala rangi.
Kupumua monoksidi ya kaboni kunaweza kusababisha
kichefuchefu, kuzimia, au kifo.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha majeraha
mabaya ya moto au kifo.
Washa na uendeshe injini nje.
Usiwashe au kuendesha injini ndani ya eneo
lililofunikwa, hata kama milango na madirisha yako
wazi.
1 Kagua kiwango cha oili (angalia Kagua na Uongeze Oili
ya Injini).
2 Hakikisha udhibiti wa kuendesha kifaa imetolewa.
3 Kalia kiti na uinue wenzo wa kurekebisha kiti JUU, uweke
inavyotakikana, na uondoe wenzo wa kufunga kiti katika
nafasi yake.
4 Weka breki ya kuegesha. Kanyaga breki ya kuegesha
kabisa, vuruta JUU kidhibiti cha breki ya kuegesha, na
uwachilie pedali ya breki.
5 Zima swichi ya PTO kwa kusukuma NDANI.
6 Weka udhibiti wa mmiminiko wa mafuta/choki upande wa
CHOKI.
7 Ingiza kifunguo katika swichi ya kuwasha na ukizungushe
upande wa WASHA/ANZISHA.
8 Baada ya injini kuwaka, zogeza udhibiti wa mmiminiko
wa mafuta/choki kwa kasi nusu. Pasha injini joto kwa
kuiendeshwa kwa angalau sekunde 30.
9 Weka udhibiti wa mmiminiko wa mafuta/choki upande wa
HARAKA.
Katika hali ya dharura injini inaweza kusimamishwa
kwa urahisi kwa kuzungusha switchi ya kuwashia
kwenye SIMAMA. Tumia njia hii tu katka hali za dharuara.
Kwa uzimaji wa kawaida wa injini fuata taratibu ziliztolewa
katika Kuzima Trekta na Injini.
KUMBUKA: Ikiwa injini haitawaka baada ya majaribio
kadhaa, wasiliana na muuzaji aliyeidhinishwa.
Kuendesha Trekta
1 Kalia kiti na urekebishe kiti ili uweze kufikia vidhibiti
vyote vizuri na uone onyesha la dashibodi vizuri (angalia
Vipengele na Vidhibiti).
2 Weka breki ya kuegesha. Kanyaga breki ya kuegesha
kabisa, vuruta JUU kidhibiti cha breki ya kuegesha, na
uwachilie pedali ya breki.
3 Hakikisha swichi ya PTO imeondolewa.
4 Washa injini (angalia Kuwasha Injini).
5 Ondoa breki ya kuegesha. Kanyaga pedali ya breki
kabisa, bonyesha CHINI kwenye udhibiti wa breki ya
kupakia, na uwachilie pedali ya breki.
6 Kanyaga pedali ya kuenda mbele ili uende mbele.
Wachilia pedali ili usimame. Kumbuka kwamba
unapokanyaga pedali chini zaidi ndivyo trekta itaenda
haraka.
7 Simamisha trekta kwa kuwachilia pedali za udhubiti wa
kasi, ukiweka breki ya kuegesha, na usimamishe injini
(angalia Kusimamisha Trekta na Injni).
Kukata nyasi
1 Weka urefu wa kukata kwa kiwango unachotaka ukitumia
wenzo wa urefu wa kukata nyasi (angalia Vipengele na
Vidhibiti).
2 Weka breki ya kuegesha. Hakikisha swichi ya PTO
imeondolewa.
3 Washa injini (angalia Kuwasha Injini).
4 Weka udhibiti wa mmiminiko wa mafuta/choki upande wa
HARAKA.
5 Weka PTO ili uwashe bapa za kukata nyasi.
6 Toa breki ya kuegesha kisha uanze kukata nyasi.
7 Ukimaliza kukata nyasi, zima PTO.
8 ZIMA injini (angalia Kuzima Trekta na Injini).
ONYO
Injini itazima ikiwa pedali ya kurudi nyuma itakanyagwa
wakati PTO imewashwa na RMO haijawashwa.
Mwendeshaji anafaa awe akizima PTO wakati wote
kabla ya kuendesha kwenye barabara, vinjia, au eneo
lolote ambalo linaweza kutumiwa na magari. Kupoteza
nguvu kwa ghafla kunaweza kusababisha hatari.

Related product manuals